Mbunge Wambugu Ngunjiri alaumu polisi

KTN News Dec 09,2019


View More on KTN Leo

Mbunge wa Nyeri mjini Wambugu Ngunjiri sasa amewanyoshea kidole cha lawama maafisa wa polisi akiwalaumu kwa kile ametaja kuwa utepetevu kufuatia vurumai zilizoshuhudiwa Nyeri hapo jana kwenye hafla ya kuchangisha fedha iliyohudhuriwa na naibu rais William Ruto katika shule ya upili ya wavulana ya giakanja. Vurugu hiyo inasemekana kuwahusisha wakazi wanaoaminika kuwa wafuasi wa mbunge huyo waliokuwa wakikabiliana na kundi jingine likiaminika kuwa la wafuasi wa naibu wa rais.