Vurumai Nyeri: Makabiliano kati ya wafuasi wa Ngunjiri na wa Naibu Rais yashuhudiwa alasiri leo

KTN News Dec 09,2019


View More on Leo Mashinani

Makabiliano Makali Yalishuhudiwa Katika Shule Ya SEKONDARI Ya Giakanja Katika Kaunti Nyeri Baada Ya Mirengo Miwili Ya Kisiasa Kukabiliana Kabla Ya Hafla Ya Naibu Wa Rais William Ruto. Hafla Hiyo Ya Kuchangisha Fedha, Ilianza Kwa Ghasia, Huku Wafuasi Wa Mbunge Wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu Wakizuiliwa Kuingia Katika Eneo La Mkutano. Vuta Nkuvute Hata Hivyo Ilishuhudiwa Alipowasili Wambugu, Huku Wakaazi Waliokuwa Wamebea Rungu Na Hata Visu Wakikabiliana, Huku Baadhi Yao Wakijeruhiwa Vibaya. Wawakilishi Wadi Ni Miongoni Mwa Waliozua Rabsha Hiyo. Kikao Hicho Hata Hivyo Kiliendelea Baadaye, Huku Viongozi Wakikashifu Kilichojiri