Haji awaonya Magavana Waititu, Lenolkulal dhidi ya kuendelea na kazi zao rasmi

KTN News Dec 06,2019


View More on Dira ya Wiki

Awali Mkurugenzi Mkuu Wa Mashtaka Noordin Haji Alikuwa Ametoa Taarifa Na Kuelezea Kuwa Kuna Ushahidi Wa Kutosha Wa Kumshtaki Gavana Mike Sonko.  Kwa Mujibu Wa  Haji, Sonko Yumo Matatani Kuhusiana Na Kupotea Kwa Shilingi Milioni 357 Za Kaunti Zinazoshukiwa Kufujwa Na Gavana Huyo Pamoja Na Washirika Wake City Hall.

Isitoshe, Mkurugenzi Wa Mashtaka Ya Umma Noordin Haji Pia Alitoa Onyo Kwa Gavana Wa Kiambu Ferdinand Waititu Na Mwenzake Wa Samburu Moses Kasaine Lenolkulal Dhidi Ya Kupuuza Agizo La Mahakama Lililowazuia Kutekeleza Shughuli Rasmi Wakisubiri Kumalizika Kwa Kesi Zinazowakabili.