Shirika la Red Cross latahadharisha wanaoishi kando la mto Tana kwamba huenda watafurishwa

KTN News Dec 06,2019


View More on Leo Mashinani

Kwa mara nyingine tena shirika la red cross limeonya kwamba watu wengi wanaoishi kando kando mwa mto Tana wataendelea kufurushwa makwao kwenye siku zijazo kutokana na  kupanda kwa viwango vya mto huo huku mvua zikiendelea kushuhudiwa. Akizungumza wakati wa kutoa chakula cha msaada kwenye kambi ya ziwani ambako zaidi ya familia mia nne zimetafuta makazi,meneja wa eneo la kaskazini mashariki Mohammed Abdikadir amesema iwapo mvua hiyo itaendelea basi wengi watalazimika kuhama makwao.kufikia alhamisi wiki hii viwango vya mto huo vilikuwa vimepanga kutoka mita tatu nukta tisa hadi mita tano nukta kumi.