Margaret Nyakango aapishwa kama msimamizi wa bajeti | MBIU YA KTN

KTN News Dec 04,2019


View More on KTN Mbiu

Margaret Nyakango ndiye msimamizi mpya wa bajeti za serikali. Nyakango ameapishwa kwenye sherehe iliyoongozwa na jaji mkuu David Maraga katika mahakama ya upeo hapa Nairobi. Nyakango aliyeteuliwa na rais Uhuru Kenyatta mwezi jana anamrithi Agnes Odhiambo. Nyakango ni mhasibu na atahudumu kama msimamizi wa bajeti kwa muda wa miaka minane.