Mahakama yasitisha ada ya maegesho ya magari iliyopitishwa na serikali ya Nairobi | MBIU YA KTN

KTN News Dec 04,2019


View More on KTN Mbiu

Mahakama kuu imesitisha ada ya shilingi mia nne ya maegesho ya magari, ambayo serikali ya kaunti ya nairobi ilikuwa imepitisha kuwa itaanza kutekelezwa hii leo. Hii ni baada ya shirikisho la matumizi ya huduma na bidhaa ( COFEK) kuwasilisha kesi ya kupinga ada hiyo kupandishwa maradufu kutoka shilingi 200 hadi shilingi 400.