KUPPET yaipa wizara ya elimu makataa ya siku saba kuboresha mazingira ya kazi kwa watahini wa KCSE

KTN News Dec 03,2019


View More on KTN Mbiu

Chama cha walimu wa sekondari na vyuo, KUPPET, kimeipa wizara ya elimu na baraza la mitihani nchini makataa ya siku saba ili kuboresha mazingira ya kazi kwa watahini wa mtihani wa kcse, la sivyo waitishe mgomo. Uongozi wa chama hicho umetaja malipo duni kwa watahini na msongamano katika shule za  upili za Machakos girls na Starehe kuwa sababu kuu ya ilani yao.