Familia yaomba usaidizi baada ya mpendwa wao kuzama majini Uganda

KTN News Dec 02,2019


View More on KTN Leo

Familia moja kutoka kijiji cha Siekunya eneo la Nambale kaunti ya Busia sasa inaiomba serikali kuingilia kati ili kusaidia kuopoa maiti ya mpendwa wao aliyezama baada ya mashua yao kuzama kwenye mto Ashwa wilaya ya Pader nchini Uganda wiki moja iliyopita. Joseph Wafula mwenye umri wa miaka 42 aliyekuwa akifanya kazi kama mtaalamu wa maji alikuwa katika shughuli za kikazi eneo hilo kabla ya mashua 
yao kuzama. Mashua hiyo ilikuwa imebeba watu 4 akiwemo marehemu, ila ni wawili pekee walionusurika. Mbunge wa Nambale John Bunyasi amelaumu serikali ya Uganda kwa kujikokota katika shughuli ya kuopoa maiti ya mwendazake