Watu watano wa familia moja wafariki katika Eneo la Ngatatai Kaunti ya Kajiado

KTN News Nov 25,2019


View More on Leo Mashinani

Watu Watano Wa Familia Moja Wamefariki Usiku Wa Kuamkia Leo Kufuatia Kusombwa Na Mafuriko Katika Eneo La Ngatatai Kaunti Ya Kajiado. Miili Ya Watano Hao Waliokuwa Wakisafiri Kutoka Eneo La Namanga Kuelekea Il?Bisil Ilipatikana Majira Ya Saa Kumi Asubuhi Alfajiri. Akidhibitisha Kisa Hicho Afisa Mkuu Wa Polisi Katika Eneo Hilo David Oloro?Nyopwe Amewasihi Madereva Kuwa Makini Wanapoendesha Magari Wakati Huu Wa Msimu Wa Mvua. Aidha Amewatahadhari Wakaazi Kuwa Makini Sana Wanapovuka Mito Ambayo Imekwisha Vunja Kingo Zake. Kwa Upande Wake Kasisi Njenga Amewafariji Wanafamilia Wakati Huu Wa Majonzi. Milli Ya Watano Hao Imepelekwa Katika Chumba Cha Kuhifadhi Maiti Katika Hospitali Ya Kajiado.