Wanafunzi wanne wa kike wavumbua kifaa cha kugundua mabomu na gurunedi

KTN News Nov 14,2019


View More on KTN Mbiu

Kilichaonza kama zoezi la ziada la somo la Sayansi katika shule ya sekondari ya wasichana ya St. Thomas iliyoko kaunti ya Kilifi sasa kimeanza kuvutia makini ya jeshi la taifa. Hii ni baada ya wanafunzi wanne wa kike kuvumbua kifaa cha kugundua vilipuzi vya kutegwa ardhini au gurunedi.