12th November, 2019
Shirikisho la raga nchini kru likishirikiana na damu pevu hii leo limezindua mikakati ya kukuza raga nchini. Ushirikiano huo utaisaidia shirikisho hilo kupeleka raga katika shule za msingi mbali mbali nchini huku dhamira ikiwa ni kueneza mchezo huo nchini. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, mwenyekiti wa shirikikisho hili Oduor Gangla alisema kwamba hiyo ni hatua moja wanatumia kuwapata wachezaji ibuka nchini.