.
5th November, 2019
Chama cha ushirika cha kina mama kaunti ya Lamu kimetumia mtaji wao wa shilingi milioni 10.7 kuanzisha mradi wa bodaboda ili kuwasaidia wanachama wake kujiimarisha kiuchumi na kuboresha hali yao ya maisha. Mradi huo ambao mlezi wake ni mwakilishi wa kina mama kaunti hiyo Kapteni Ruweidda Obbo unanuia kuwafaidi zaidi ya wanachama elfu 3 wa ushirika huo walio maeneo ya Lamu Mashariki na lamu Magharibi. Tayari pikipiki mpya 60 zimenunuliwa na kusambazwa kwenye maeneo hayo huku ikitarajiwa kuwa utakuwa na faida itakayowanufaisha kina mama.