16th April, 2019
Timu ya shule ya upili ya St. Joseph Kirandich iliyoshamiri katika mashindano ya shule za upili yaliyoandaliwa mjini mombasa wanafurahi sana haswa baada ya kushamiri na sasa wanaangazia safari ya kuelekea tanzania. Walitwaa ubabe katika mchezo wa handiboli na itakuwa mara yao ya kwanza kuwakilisha kenya katika mashindano ya afrika mashariki ya upande wa shule.