16th April, 2019
Kikosi cha wanariadha wanaoishi na ulemavu kinapojiandaa kuelekea Morocco kushiriki mashindano ya kufuzu kushiriki olimpiki ya wanaoishi na ulemavu mwaka ujao, serikali ya Morocco kupitia ubalozi wao nchini, umeipa kikosi hicho ufadhili kama njia moja wapo ya kuimarisha uhusiano wema kati yao na kenya. Kikosi hicho kitaondoka nchini siku ya jumamosi alhasiri kuelekea Morocco kwa mashindano hayo.