Wakaaji wa Embakasi wafanya maandamano

KTN News Mar 27,2019


View More on KTN Leo

Vurugu zilishuhudiwa mapema leo katika eneo la embakasi mashariki kufuatia maandamano ya wakazi waliokuwa wakilalamika kuhusu barabara mbovu na uhaba wa maji. Wakazi hao wenye hasira wanadai kukerwa na mwanakandarasi aliyepewa jukumu la kujenga barabara ya embakasi?simbavilla?kayole, anayesemekana kuharibu mabomba na mifereji ya maji, hivyo kuhitilafiana na mtiiriko na usambazaji wa maji. Na sasa wamempa mwanakandarasi huyo makataa ya siku moja akamilishe kazi yote.