Waziri Fred Matiang'i ataka mavazi ya maafisa wa serikali kutengenezwa nchini Kenya

KTN News Mar 25,2019


View More on KTN Leo

Waziri wa usalama wa ndani, daktari fred matiang’i, amezitaka wizara na idara zote za serikali kukoma mara moja ununuzi wa sare na mavazi rasmi kutoka nje. Matiang’i, ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati kuu ya serikali kuhusu ustawi na utekelezaji wa miradi, amesema uagizaji wa bidhaa muhimu kama vile mavazi kutoka mataifa ya nje ni kudhoofisha uchumi wa nchi. Matiang'i aliyasema hayo alipoyatembelea makao makuu ya nys kukagua ushonaji wa sare za polisi.