Viongozi kutoka katika Kaunti ya Wajir wamekashifu kuhamishwa kwa Waziri Amina Mohamed

KTN News Mar 16,2019


View More on KTN Leo

Baadhi ya viongozi kutoka katika Kaunti ya Wajir wamekashifu kuhamishwa kwa Waziri Amina Mohamed kama waziri wa elimu na wadhifa wake  kukabidhiwa profesa george magoha.wakiongozwa na mbunge wa wajir east rashid kassim, viongozi hao wametaja mabadiliko ya hivi juzi yaliofanywa na rais uhuru kenyatta  katika baraza la mawaziri kama hujuma kwa jamii ya kuhama hama na wametishia kuwashinikiza wabunge wenzao kutoidhinisha uteuzi wa magoha. Wanadai magoha hakuwajibika alipokuwa mwenyekiti wa baraza la kitaifa la mitihani nchini.