.
12th March, 2019
Serikali imetoa zaidi ya bilioni 12 ya malipo ya wazee na makundi ya wasiojiweza katika jamii chini ya mradi wa "inua jamii". Zaidi ya watu elfu mia saba watapokea fedha hizo kutoka kwa serikali ambazo hazijalipwa kwa miezi sita. Serikali ilisitisha malipo kwa kipindi hicho ili kuwapa nafasi walengwa kujisajili kwenye mfumo mpya wa programu hiyo. Katibu wa kudumu katika wizara ya leba nelson marwa ameamuru benki kutoa malipo hayo kwa wanaolengwa pindi tu zitakapopokelewa. Marwa ameonya kuwa hatua kali itachukuliwa kwa benki zitakazo kaidi amri hii.