Mwanamume wa miaka 40, Sylvester Bwire ashukiwa kumnajisi msichana wa miaka tisa

KTN News Feb 25,2019


View More on KTN Leo

Mwanamume wa miaka arobaini anatarajiwa kufikishwa mahakamani huko Busia kwa tuhuma za kumnajisi msichana wa miaka tisa na kumpa zawadi ya shilingi 130 ili anyamaze na kutosema lolote kuhusu tendo hilo. Sylvester Barasa Bwire, anadaiwa kumnajisi msichana huyo katika kituo cha muluanda alipokuwa amekwenda kununua mafuta taa na badala yake akamshawishi hadi chumbani mwake na kuutekeleza uovu huo.