Watu 4 wamepoteza maisha yao kutokana na ajali katika barabara ya Kachibora

KTN News Feb 25,2019


View More on KTN Leo

Watu 4 wamepoteza maisha yao kutokana na ajali ya barabarani iliohusisha gari la serikali na bodaboda barabara ya Kachibora inayoelekea Kitale sehemu ya Cherangany kaunti ya trans nzoia. Waliopoteza maisha yao ni mhudumu wa bodaboda na abiria 3 ambao ni mwanamke mmoja na watoto 2. Wakazi waliokua na hasira waliliteketeza kwa moto gari hilo kutoka idara ya ujasusi nchini nis wakilalamikia mauaji hayo. Dereva wa gari hilo alifaulu kukimbia, baada ya walioshuhudia kudai kuwa alikua akiliendesha kwa mwendo wa kasi.