Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko abuni mpango wa kuongeza viwango vya misitu nchini

KTN News Feb 23,2019


View More on KTN Leo

Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko ameyataka mashirika ya umma yanayomiliki ardhi isiyotumika kutumia ardhi hiyo kupanda miti ili kuongeza viwango vya misitu nchini. Tobiko alikuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzuru msitu wa Better Globe uliopo katika eneo la bwawa la Kiambere kaunti ya kitui.