Mwanakandanda Mashuhuri Joe Kadenge anaendelea kupata nafuu katika hospitali ya Nairobi

KTN News Feb 18,2019


View More on Sports

Mwanakandanda Mashuhuri Joe Kadenge anaendelea kupata nafuu katika hospitali ya Nairobi. Kadenge alipatwa na kiarusi baada ya kupata habari kuwa bintiye ameaga dunia jumatano iliyo pita. Gwiji huyo ameondolewa katika wodi ya wagonjwa maututi na kupelekwa katika wodi ya jumla anakoendelea kupata matibabu.  Kadenge anatarajiwa kuondoka hospitalini siku ya jumatano. Mwenda zake bintiye anazikwa leo nchini Amerika.