Makala ya pili ya mashindano ya chipukizi ya raising stars yalingóa nanga

KTN News Feb 11,2019


View More on Sports

Makala ya pili ya mashindano ya chipukizi ya raising stars yalingóa nanga hiyo jana katika shule ya upili ya hillcrest mjini nairobi. Kwenye kitengo cha vijana wasiozidi miaka 13, timu ya express soccer academy iliicharaza syokimau tatu bila jibu huku ligi ndogo ikiichabanga syokimau nne kavu. Katika kitengo cha walio chini ya miaka 9, express 1 waliwanyofoa ligi ndogo 1 saba kwa moja nao blue bombers wakaambulia sare tasa na consolata. Michuano hiyo inayoshirikisha timu 40 inachezwa kila siku ya jumapili kuwapa fursa wachezaji chipukizi kukuza talanta zao.