.
7th February, 2019
Wenyeji wa eneo la kitui mashariki wana kila sababu ya kutabasamu baada ya mbunge wao nimrod mbai kuanzisha harakati za kufungua shule ambayo ilifungwa miaka 27 iliyopita kutokana na utovu wa usalama uliosababishwa na wizi wa mifugo.Shule hiyo ya engamba inayopatikana mpaka wa kaunti ya kitui na tana river ilifungwa baada ya wafugaji kuivamia na kumuua mwalimu mkuu.wanafunzi kadhaa na wafanyakazi Wengine wa shule pia walijeruhiwa.tangu mwaka 1992, shule hiyo ambayo ilikuwa na wanafunzi 300 imesalia mahame.baada Ya kufungwa elimu iliathirika pakubwa kutokana na kukosekana kwa shule nyengine karibu.