7th February, 2019
Ni afueni kwa gavana wa homabay Cyprian Awiti baada ya mahakama ya upeo kuidhinisha ushindi wake.Jaji wa mahakama ya upeo Profesa Jackton Ojwang aliyesoma uamuzi huo amesema kuwa mahakama za chini hazikuzingatia ifaavyo vipengee muhimu katika kesi hiyo. Mshindani wa awiti katika kinyanganyiro cha kiti cha ugavana Oyugi Magwanga ambaye alikuwa mbunge wa kasupul aliwasilisha kesi mahakamani mwezi septemba mwaka 2017 akipinga ushindi wa awiti uliotangazwa na tume ya uchaguzi.Mahakama kuu na mahakama ya rufaa zilibatili ushindi wa awiti kwa kigezo kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na dosari.awiti kisha alielekea mahakama ya upeo ambayo imetoa uamuzi ambao umeidhinisha ushindi wake.magwanga aliwania kiti hicho Akiwa mwaniaji wa kujitegemea huku awiti akigombea kupitia tiketi ya ODM