31st January, 2019
Visa vya wizi wa kahawa katika eneo la kati ya taifa huenda vikawekwa katika kaburi la sahau iwapo hatua zilizowekwa na kamati ya usalama katika eneo hilo vitatiliwa maanani. Akizungumza kwenye kikao na wanahabari mjini nyeri, kamishna wa eneo la kati ya kenya wilfred nyagwanga amesema kuwa maafisa wa usalama watahusishwa katika usafirishaji wa zao hilo ili kupunguza visa vya wizi vinavyotokea barabarani. Aidha kamishna huyo aligusilia swala la usalama katika eneo hilo, huku akieleza kuwa zipo mipango maalum za kupambana na visa vya wakaazi kujiunga Na makundi haramu