Viongozi wapendekeza kutangazwa kwa saratani kuwa janga la taifa

KTN News Jan 30,2019


View More on Leo Mashinani

Gavana wa kaunti ya Makueni Kivutha Kibwana ametoa wito kwa wabunge kubuni mswada utakaoisukuma serikali kutangaza saratani kuwa janga la taifa. 

Pendekezo la Kibwana lilipigwa jeki na mbunge wa kwanza Ferdinand Wanyonyi ambaye ameitaka serikali kutenga kiasi fulani cha pesa kwa matibabu ya saratani katika kaunti zote 47. 

Walikuwa wakizungumza katika kaunti ya Machakos.