23rd January, 2019
Jopo kazi lilioundwa na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga kuangalia jinsi ya kuleta uwiano wa kitaifa katika utawala na uongozi (building bridges initiative ), limetua mjini Isiolo kukusanya maoni ya wananchi.
Washiriki kwenye mawasilisho hayo wanasisitiza usawa wa ugavi wa rasilmali na kuondoa ukiritimba wa uongozi wa taifa. Seneta wa kaunti ya Garissa Yusuff Haji aliliongoza jipo hilo.