23rd January, 2019
Wakulima wa mahindi katika kaunti ya Samburu sasa wanalalamikia ukosefu wa soko kwa mazao yao.
Wakulima hao wamelalama kwamba bei ya shilingi elfu moja mia tano kwa kila gunia la mahindi ni hasara kwao na kutaka serikali kuwakumbuka kwa kuwapa bei nzuri kupitia halmashauri ya nafaka na mazo, NCPB.
Aidha wakulima hao wanasema kwamba serikali imeangazia sana eneo la bonde la ufa na kusahau maeneo mengine yanayopanda mahindi vile vile.