18th January, 2019
Mzozo wa ardhi umezuka katika soko la olomunyi huko kajiado ya kati, ambapo wanawake wanawalaumu baadhi ya maafisa wa serikali ya kaunti ya kajiado kwa kuwanyima haki ya kuendelea kulitumia soko hilo ambalo wamelitegemea kwa miaka mingi sasa. Hii ni baada ya wanawake hao kuandamana na kuwasilisha malalamiko yao kwa serikali ya kaunti, ambapo ahadi walizopewa wanadai hazijatimizwa. Licha ya masoroveya kutum,wa katika eneo hilo ili kutafuta suluhu, hali ingali ni ile ile.