Mvulana wa miaka 15 amezama maji na kufariki katika bwawa la Barotio Kericho alipokua akiogelea

KTN News Jan 14,2019


View More on Leo Mashinani

Mvulana wa umri wa miaka 15 amezama maji na kufariki wakati alipokuwa akiogelea katika bwawa la Barotio huko Kericho. Mwenda zake emmanuel kipyegon aliyekuwa akisubiri kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya upili ya Kapcheplanga anasemekana kutaka kujiburudisha nyakati za mwisho mwisho nyumbani kabla ya kuanza maisha mapya ya elimu ya sekondari ila maji yakamzidi pale alipoogelea hadi  kati kati ya dimbwi hilo. Chifu wa kata ya masaita  simeon mureu alithibitisha maafa hayo na akasema kwamba iliwachuku wapiga mbizi wa kujitolea zaidi ya saa kumi na  sita kuutafuta mwili wa marehemu.