Shirika la KENPHIA na serikali ya Kaunti ya Samburu wameanzisha mpango wa kuwapima wenyeji

KTN News Jan 11,2019


View More on Leo Mashinani

Shirika la KENPHIA yaani kenya population based hiv impact assesment kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya samburu wameanzisha mpango wa kuwapima wenyeji kubaini iwapo wana virusi vya hiv, hepatitis b na kisonono. Naibu gavana julius lesseto amesema kuwa mpango utahakikisha kuwa idadi kubwa ya watu wamepimwa magonjwa hayo akitaja kuwa chini ya asilimia kumi ya watu na haswa kina mama waja wazito wamepimwa virusi vya hiv. Vipimo hivyo vitasaidia serikali ya kaunti kuweka takwimu za watu wanaougua maradhi hayo.