Msichana aliyepata 392 aingia mafichoni ili kwepa ukeketaji Kuria

KTN News Dec 26,2018


View More on Leo Mashinani

Msichana mwenye umri wa miaka kumi na miwili aliyepita mtihani wake wa KCPE mwaka huu na kupata alama 392 huenda asijiunge na kidato cha kwanza baada ya kuingia mafichoni ili kuepukana na ukatili wa ukeketeaji. Sarah Gasaya kutoka Kaunti ndogo ya Mabera eneo bunge la Kuria magharibi katika kaunti ya Migori, amepokea barua ya kujiunga na shule ya upili ya pangani ila alilazimika kutorokea kwa dadaye nyanyake alipopata habari kuwa huenda wakakeketwa kwa pamoja na dada zake wawili. Dadake sarah Catherine bhoke mwenye umri wa miaka kumi na saba na Dorcas Nkaina mwenye umri wa miaka kumi na sita waliweza kukeketwa kwa lazima na wanakikiji chao baada ya kukwepa wembe kwa zaidi ya miaka kumi