Waziri wa Usalama wa Ndani Matiang'i atoa onyo kali kwa wanaokata miti bila idhini

KTN News Dec 19,2018


View More on KTN Leo

Waziri wa Ulinzi wa Ndani Fred Matiang’i amewaonya wananchi wote wanaokata miti bila idhini na kuwataka machifu na manaibu wake kuhakikisha wanakamatwa. Haya yanajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta kupiga marufuku ukataji wa miti huku ikiwa ni chanzo cha kupunguza ukubwa wa misitu yetu. Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa upandaji miti uitwao “Greening Kenya”. Huu ni mpango wa ushirikiano baina ya wizara ya vijana, usalama wa ndani na ile ya misitu.