×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Afisa wa polisi adaiwa aliwamiminia risasi na kuwaua watu watano Kolongolo, Trans Nzoia

17th December, 2018

Kisa cha hapo jana ambapo afisa mmoja wa polisi huko Kolongolo kaunti ya Trans Nzoia anadaiwa aliwamiminia risasi na kuwaua watu watano, kimeshtumiwa na uongozi wa kaunti hiyo. Gavana Patrick Khaemba amekemea kisa hicho kilichowaacha watu wengine na majeraha, pale ambapo makabiliano yalizuka kati ya raia na maafisa wa polisi. Wito umetolewa wa hatua kuchukuliwa dhidi ya mhusika wahusika. Makabiliano hayo yalitokana na mzozo katika familia moja, ambapo polisi walipojaribu kuingilia kati, ndipo raia wakaanza kuwakaripia maafisa hao. Watu wawili walikufa papo hapo huku wengine watatu wakifariki walipokuwa wakipokea matibabu hospitalini.

.
RELATED VIDEOS