3rd December, 2018
Prof. Patrick Kafu ni msomi wa kutajika katika masuala ya Taaluma ya ualimu. Msomi huyo anayesifiwa sana na walimu waliopitia mikononi mwake katika vyuo vikuu vya humu Nchini, si mwalimu darasani tu, bali pia katika nyanja ya kilimo mashinani. Tulimpata katika shamba Lake huko Mumbu, Kitale akishirikiana na mkewe Bi Grace Namikoye Kafu wakishirikiana kwenye kilimo cha mmea wa Sun flower, ambapo kwa sasa wao ndio wauzaji wakuu wa mafuta yanayotokana na sun flower katika eneo hilo.