Sherehe za kuidhinisha siku ya Ukimwi zafanywa katika sehemu mbalimbali nchini

KTN News Dec 01,2018


View More on KTN Leo

Maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini yakiwa yametajwa kuwa juu miongoni mwa vijana wa umri wa kati ya miaka kumi na nane na ishirini na nne, juhudi zimeendelea kuwekwa kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa kujua hali yao sawa na kuwakumbatia wanaoishi na virusi vya Ukimwi. Kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani mwanahabari Sycilia Wakesho Mathuva alihudhuria warsha ya ‘rangi’ almaarufu kama colour festival ambako vijana walimiminika kupokea mafunzo kuhusiana na siku hii.