26th November, 2018
Huku zikiwa zimebakia siku kumi na moja tu kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya taifa kung'oa nanga , klabu ya gor mahia imewasajili wachezaji nane wapya ikiwemo kenneth muguna kutoka fk tirana ,pascal ogweno kutoka kariobangi sharks na shafik batambuze kutoka singida ya tanzania.aidha gor mahia imekanusha madai kwamba walimpiga kalamu kocha wao dylen kerr. Gor mahia inajiandaa kushiriki mchuano wa klabu bingwa barani dhidi big bullets ya malawi jumatano ugani kasarani.