18th November, 2018
Msako mkali unaendelea katika maeneo ya kaunti za nandi na Kisumu kumtafuta mtu aliyejihami kwa panga ambaye anasadikika kumuua kwa kumkatakata mfanyikazi katika shamba la aliyekuwa Effie Owuor.
Mwanawe wa kiume alijeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo la hapo jana. Kamanda wa polisi katika eneo hilo Leornard katana ambaye alizuru eneo la tukio amesema wanachukulia kisa hicho kama uhalifu wa kawaida na sio mzozo wa mara kwa mara ambao hujitokeza katika eneo la mpakani kati ya kaunti ya Kisumu na Nandi.
Haya na mengine mengi katika makala ya Mbiu ya KTN