6th November, 2018
Halmashauri ya mfuko wa kuhakikisha usalama wa chakula nchini (strategic food reserve fund?SFRF) imeidhinisha halmashauri ya nafaka na mazao NCPB kununua mahindi kutoka kwa wakulima kwa bei ya shilingi 2300 kwa gunia la kilo tisaini. Akitoa tangazo hilo, mwenyekiti wa halmashauri hiyo DR. Noah Wekesa amesema kuwa Wizara ya Fedha inatarajiwa kutoa shilingi bilioni 5.7 kwa ajili ya kununua magunia milioni 2.5 kutoka kwa wakulima wakati huu wa msimu wa mavuno. Hata hivyo wakulima wanatarajiwa kupinga pendekezo hilo hasa ikizingatiwa kuwa mahindi hayo yalinunuliwa kwa zaidi ya shilingi alfu tatu kwa gunia msimu uliopita.