Mjane wa Aboud Rogo aachiliwa

KTN News Oct 05,2018


View More on Dira ya Wiki

Mjane wa aliyekuwa mhubiri wa Kiislamu Aboud Rogo, Haniya Sagar amewachiliwa huru baada ya kuhukimiwa kifungo cha miaka kumi gerezani kwa kuhusishwa na shambulio la kigaidi katika kituo kimoja cha polisi mjini Mombasa mwaka 2016. 

Mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu, hania alikata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyotolewa hakimu wa mahakama ya Mombasa, Diana Mochache baada ya kupatikana na hatia ya kutotoa taarifa kuhusu magaidi waliokivamia kituo hicho cha polisi.

Katika uamuzi wake, hakimu Mochache alisema hania alikuwa akiwasiliana mara kawa mara na magaidi hao watatu; Tasnim Yakub, Ramla Abdirahman Hussein na Maimuna Abdirahman ambao waliuwawa na maafisa wa polisi dakika chache baada ya kuvamia kituo cha polisi cha Central. 

Mumewe Aboud Rogo aliuwawa na watu wasiojulikana Agosti mwaka 2012 na alidaiwa kuhusishwa na visa vya kigaidi nchini pamoja na mtandao wa Al Quaeda.