3rd October, 2018
Waziri wa Afya Sycil Kariuki amesema kuwa bei ya dawa nchini ni ya juu mno ikilinganishwa na maeneo mengine duniani licha ya kuwa dawa zenyewe ni sawa kimatumizi. Akizungumza muda mfupi uliopita kariuki amesema kwamba sekta ya afya inatakiwa kupigwa darubini kali ili kujua chanzo cha dawa kutopatikana ama kutoweka katika vituo vya afya vya umma.