28th September, 2018
Watazamaji wa runinga ya KTN Home watapata burudani zaidi, baada ya kampuni ya Standard Group kutia saini mkataba wa kuonesha mechi moja ya ligi kuu ya uingereza na kampuni ya Kwesse Sports.
KTN itaonesha mechi hizi kila jumamosi saa kumi na moja kamili.
Wikendi hii KTN itapeperusha moja kwa moja mechi kati ya mabingwa Manchester city na Brighton & Hove Albion ambao wanashikilia nafasi ya 13 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza.