26th September, 2018
Msaidizi wa gavana wa kaunti ya Migori Michael Oyamo, amerejeshwa tena katika mahakama ya Milimani kujibu mashtaka ya mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno. Alikanusha mashtaka hayo mbele ya jaji wa mahakama kuu Jessy Lessit ambapo ataendelea kuzuiliwa rumande hadi tarehe nane mwezi ujao .