24th September, 2018
Zaidi ya watu 600 wanaoishi na ulemavu walikongamana katika uwanja wa machakos people’s park katika kaunti ya machakos ili kusherehekea uwezo walionao katika tamasha zilizopewa jina la uhai?festival. Washiriki wataonesha umaahiri wao katika michezo mbali mbali ikiwemo mazungumzo,mpira wa vikapu, voleboli, ndondi kwenye viti, ruji ya wasioweza kusikia, sarakasi pamoja na maonesho ya urembo na fasheni.tamasha hizi zitachukua siku mbili na lengo kuu haswaa ni kupigana na unyanyapaa dhidi ya ulemavu. Gavana wa machakos Alfred Mutua alifungua tamasha hizo.