Wafuasi wa Obado waandamana katika eneo la Uriri

KTN News Sep 23,2018


View More on KTN Mbiu

Wafuasi wa Gavana wa kaunti ya Migori anayekabiliwa na utata Okoth Obado wamefanya maandamano hivi leo katika eneo la Uriri kupinga hatua ya kuzuiliwa kwake kuhusiana na  uchunguzi unaoendelea wa mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno. 

Wafuasi hao ambao walijumuisha watu wa familia ya Obado waliandamana kutoka kijiji chake cha Rapogi hadi mjini Uriri wakitilia shaka hatua ya tume ya kupambana na ufisadi EACC kupiga tanji akaunti zake.