18th September, 2018
Bingwa mara tatu wa mashindano ya tenisi ya Kenya open Shufaa Changawa amefuzu robo fainali ya mashindano hayo kwa kumbwaga rose wanjala kwenye mechi iliyochezwa uga wa nairobi club. Shufaa aliandikisha ushindi wa seti mbili za 6?0 na 6?1 huku kakake ismail changawa ambaye amenyakua taji hilo mara nne akimcharaza mjerumani christian vatar katika seti mbili za 6?2 na 6?3 kujikatia tiketi ya raundi ya tatu. Katika mechi nyengine iliyochezwa leo, ibrahim kibet alimlaza brandon sagala seti mbili mtungi za 6?3 na 6?3.