18th September, 2018
Kariobangi sharks wamewaduwaza AFC Leopards mabao matatu kwa moja kwenye mechi ya ligi kuu nchini iliyochezwa leo uwanjani kenyatta mjini machakos. Mshambuliaji george abege alifunga mabao mawili kwa mpigo huku duke abuya akiongeza moja kuwapa sharks ushindi wao wa nne mfululizo katika ligi kuu. Whyvonne issuza aliwafungia ingwe bao lao. Ushindi huo umewaacha sharks katika nafasi ya sita kwa alama 46 huku leopards wakiwa kwenye nafasi ya tatu kw aalama 51.