18th September, 2018
Mamlaka ya kutunza mazingira nchini nema imetoa onyo kali kwa wafanyabiashara wanaoingiza mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku nchini kupitia mipaka ya namanga na loitoktok kutoka nchi jirani ya tanzania. mkurugenzi wa nema eneo la kajiado godfrey wafula amsema licha ya hatua ya nema kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo nchini, mataifa jirani ambayo mifuko ya plastiki haijapigwa marufuku bado ni kizingiti kikuu kwa kuwa wafanyabiashara bado hupenyeza na kuingiza mifuko hiyo nchini kupitia mipakani.