17th September, 2018
Timu nane zitashiriki katika makala ya kwanza ya Mashindano ya Ligi ya Raga ya Vyuo Vikuu nchini yatakayong'oa nanga tarehe 29 mwezi huu hadi tarehe 27 oktoba papa hapa jijini nairobi. Timu za vyuo vikuu vya nairobi, kenyatta na egerton pamoja na nyinginezo zitashiriki michuano hio huku lengo kuu la mashindano hayo likisalia kukuza talanta kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka ishirini na mitano waliomo vyuoni.